Breaking News

Thursday

DAKTARI AJINYONGA NA KUFA NDANI YA GESTI HUKO MOROGORO


DAKTARI wa meno Anorld Rimo (umri wa miaka kati ya 30 hadi 40) wa hospitali ya Sabasaba manispaa ya Morogoro, amekutwa amejinyonga katika nyumba ya kulala wageni ya Camel iliopo Kihonda. Kamanda wa polisi mkoani hapa Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 22 saa 10 alfajiri katika nyumba hiyo ya kulala wageni. Alisema Daktari huyo alikuwa amepanga katika nyumba hiyo katika chumba namba 2, na kukutwa amejinyongea dirishani kwa kutumia foronya za mto pamoja na taulo. Ameeleza kuwa usiku wa kuamikia siku hiyo marehemu alikwenda katika sehemu ya mapokezi ya nyumba hiyo na kufanya fujo na kuonesha sehemu zake za siri kuwa hazifanyi kazi.

 Kamanda huyo alisema marahemu alikuwa peke yake katika chumba hicho na haikufahamika mara moja anaishi wapi. Chanzo cha kujinyonga hakijajulikana na polisi wanaendela na uchunguzi.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Chapisho Lililoangaziwa

WEDDING PARTY PHILLIPO AND LUSIO

PHILLIPO & LUSIO WEDDING PARTY: STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING MC & MUSIC BY MC SIMBA COMPANY 0715 501 059 ...

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

67157
Powered by Blogger.

Pages