Mbunge wa Mbeya mjini ambaye pia ni msanii wa bongo flava , mh.Joseph Mbilinyi
amepata ajali hivi punde katika eneo la kasheki wilayani Hanan'g akielekea
Arusha mjini.
Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu alikuwa akielekea Arusha mjini
kuungana na wabunge wengine katika shughuli ya kuwaaga marehemu waliolipukiwa na bomu kwenye mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki
iliyopita.
katika ajali hiyo hakuna mtu aliye jeruhiwa mbunge huyo yupo
salama kabisa,gari la sugu limeharibiwa vibaya baada ya kugonganana basi
hilo la abiria.
*ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU*
0 comments:
Post a Comment