Mabinti wa wili wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za
kulevyazenye thamani ya zaidi ya bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitoka
Tanzania.
Akizingumza na mwandishi wetu jana,kamanda wa polisi
ktengo cha kupambana na dawa za kulevya,
Geofrey Nzoa, alisema hajafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kua ni Agnes
Jerald(MASOGANGE) ambaye alisema hajapiga hesabu za umri wao, ili alizaliwa
mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema
amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 24. Wawili hao bado
waendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika kusini.
Alisema Jeshi la
polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama
dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakua ndiyo amiliki
wa dawa hizo.
Jumapili iliyopita mtandao huu ulipata taarifa za
kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya crystal methamphetamine zenye thamani
hiyo nchini Afrika kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili
walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la
Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliapita wakitokea Tanzania.
Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa mamlaka ya mapato ya Afrika kusini wakiwa na masanduku
sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo
pia zinajulikana kama “TIK” zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni
42 sawa n ash. Bilioni 6.8
Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo
linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28 mwaka
huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulevya hivi sasa ni janga nchini.
Alisema kumekua na wimbi kubwa la watanzania
wanaojiiongiza katika biashara za haramu
ya madawa ya kulevya ndani na nje ya nchi
na kwamba katika cha miaka mitano
iliopita watuhumiwa 10799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.
Pia alisema katika kipindi hicho Watanzania 240
walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu
taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na
masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.
Panda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji
mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na
Tanzania.
Alisema hivi sasa mikate maandazi na askrimu
zinazouzwa kwenye shule za msingi zimewekwa dawa za kulevya.
Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule
za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu ikiwemo kuingia darasani
wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe
kifuani.
Maelezo kwa hisani ya NIPASHE
0 comments:
Post a Comment