KLABU ya Levante ya Hispania inamtaka mshambuliaji 'aliyefulia' Arsenal, Marouane Chamakh. Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Morocco anauzwa, lakini Levante inataka kumnunua kwa Pauni Milioni 1 tu.
Arsenal ilimsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 bure kutoka Bordeaux, lakini alikuwa analipwa kiasi cha Pauni 65,000 kwa wiki.
Kiwango kibovu: Marouane Chamakh, kulia, hajaonyesha matumaini yoyote tangu ajiunge na Arsenal
Mshambuliaji huyo aliwasili Emirates kama mchezaji huru mwaka 2010 alitarajiwa kuwa mmoja wa wafungaji tishio, lakini amefeli hata alipopelekwa kwa mkopo West Ham msimu uliopita na kuufanya mustakabali wake uwe mbaya Ligi Kuu ya England.
***ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU***
0 comments:
Post a Comment