DAVID BECKHAM anaipa nafasi Manchester United kutetea taji lake la Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu licha ya ujio wa Jose Mourinho.
Mourinho amekuwa akipewa nafasi zaidi ya kuiwezesha Chelsea kutwaa kombe, lakini mkongwe huyo wa United anaamini timu yake ya zamani itatwaa ubingwa ifikapo mwisho wa msimu.
Becks amesema: “Utakuwa ni msimu wa kuvutia hasa kwa kuzingatia mabadilko mengi yaliyotokea miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu.
“Jose (Mourinho) amerejea na hilo ni jambo zuri. Kutakuwa na ushindani sana, lakini bado nadhani Manchester United itatwaa taji.”
Beckham anamkingia kifua Moyes kuwa ataendelea kuiletea mafanikio United baada ya kuondoka kwa Alex Ferguson.
Nyota huyo wa zamani wa England aliongeza: “Nina uhakika atafuata nyayo zake, ni mmoja kati ya mameneja ambao muda wote huwa hawaoni uvivu kunyanyua simu zao na kuongea na Ferguson.
“Kwa vyovyote vile ingekuwa ni jambo gumu kwa yeyote ambaye angemrithi Ferguson kutokana na mengi aliyoyaleta Manchester United.
“Lakini baadhi ya wachezaji bado wapo na nina uhakika wengine wachache wataongeza wiki chache zijazo. Kuwa meneja wa United ni heshima kubwa.
0 comments:
Post a Comment