DR.SALIM AHMED SALIM |
WAZIRI Mkuu mstaafu Dk. Salim Ahmed Salim, amevionya vyombo vya dola kuwa matumizi ya nguvu dhidi ya wananchi ni kiashiria cha uvunjifu wa amani.
Dk. Salim ameeleza masikitiko yake kuhusu uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani, zikiwemo kauli za viongozi na kuitaka jamii kupambana navyo kwa kudumisha misingi ya amani ambayo ni upendo, kuheshimiana na kuvumiliana.
Mwanadiplomasia huyo wa kimataifa alisema hayo Dar es Salaam jana alipozungumza na Tanzania Daima Jumatano wakati wa kongamano la kutafakari amani ya nchi lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).
![]() |
WAZIRI MKUU PINDA. |
Kauli ya kiongozi huyo mashuhuri
Afrika ilikuja baada ya kutakiwa kutoa maoni yake kuhusu kauli ya Waziri Mkuu
Mizengo Pinda aliyoitoa hivi karibuni bungeni, akiwar
uhusu
askari polisi kuwapiga wananchi aliodai wanavunja sheria.
Pinda
alitoa kauli hiyo siku chache baada ya bomu kutupwa kwenye mkutano wa CHADEMA
wa kumalizia kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani mjini Arusha kwenye Uwanja
wa Soweto.
“Mimi
nadhani nguvu ya dola siku zote itumike kwa maslahi ya wananchi… wakati
mwingine mazingira yanakuwa magumu mtu anaudhika, lakini kitu muhimu popote
pale duniani nguvu ya dola isipotumika kwa maslahi ya wananchi itavuruga amani.
“Tujifunze
kwamba bila amani, bila utulivu hakuna kinachofanyika. Vurugu katika jamii ni
mbaya, hebu tujifunze kwa nchi za wenzetu zinavyovurugana… amani ni kitu muhimu
kwa familia zetu, watoto wetu na jamii nzima.
“Lazima
tuheshimiane, tumefika kama kisiwa cha amani kwa kuheshimiana, tusibaguane,
tupambane na viashiria vya uvunjifu wa amani,” alisisitiza Dk. Salim aliyepata
kuwa balozi wa Tanzania kwenye nchi mbalimbali.
Aidha,
alionya matumizi ya nyumba za ibada yanayofanywa na baadhi ya wanasiasa nchini
na kusema si vema kupeleka siasa, huku akitaka viongozi wa dini na wanasiasa
watimize wajibu wao kila mmoja kwa nafasi yake bila kuingiliana.
Naye
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo,
Profesa Elisante ole Gabriel aliwataka viongozi wa dini kutoshabikia siasa na
kuwaonya viongozi wanaopeleka siasa kwenye nyumba za ibada.
“Viongozi
wa dini watambue nafasi yao katika kudumisha amani bila kushabikia,” alisema
mkurugenzi huyo na kuongeza kwamba wanapofanya hivyo wanaashiria uvunjifu wa
amani kwa sababu dini na siasa ni mambo tofauti.
Gabriel
alishauri kuwepo na mafunzo maalumu kwa wanasiasa ya jinsi ya kuzungumza
jukwaani huku akisisitiza kwamba yanayotokea Tanzania na Afrika nzima ni
matokeo ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila kujiandaa kisaikolojia.
Alivitaja
viashiria vya uvunjifu wa amani kuwa ni kutoaminiana kwa viongozi, wananchi na
wanasiasa jambo linalowafanya kila mmoja kumlalamikia mwenzake.
“Tusibaguane
ingawa kwa sasa ubaguzi upo kwenye siasa. Ipo siku tutabaguana dhahiri, naamini
tofauti za kisiasa ni njia rahisi ya kupoteza amani yetu. Ubaguzi wa kidini na
kikabila utatupeleka pabaya,” alisema.
Alishauri
TCD iendelee kuwezeshwa kwa gharama yeyote ili kiwe chombo cha kuwakutanisha
wanasiasa na serikali katika kuimarisha umoja, mshikamano na kuaminiana kwa
mustakabali wa amani ya Tanzania.
Alichagiza
kwamba upo uwezekano wa chama kingine kuingia madarakani, lakini sio kwa
kukidharau chama kinachotawala huku akisisitiza kwamba uwezekano wa chama
kimoja kukaa madarakani muda mrefu upo ila sio kutawala milele.
Naye
Mwenyekiti wa TCD, James Mbatia, aliwataka wanasiasa wasijione muhimu zaidi
kuliko Watanzania wengine, hivyo kila wanachokifanya lazima kiwe kwa maslahi ya
wote.
Mbatia
alisisitiza kwamba viongozi wa dini hawapendi kuona polisi wakiwalinda wakati
wanawafundisha neno la Mungu waamini wao, hivyo kuwataka wanasiasa wasiwe
chanzo cha vurugu nchini.
Naibu
Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, alisema iwapo
mifumo thabiti ya utoaji haki haijengwa na haki ikaonekana kutendeka, bado
amani ya nchi itaendelea kuwa shakani.
“Hata
TCD wakiitisha makongamano kama haya mara 10,000 wakajadili amani, kama
viongozi wa serikali hawapo tayari kuiweka mifumo thabiti ya kuifanya haki
itendeke na ionekane, hayo makongamano hayatafanikiwa.
“Watawala
wanataka kuiendesha nchi kwa kubahatisha, jambo ambalo ni hatari kwa amani ya
nchi badala yake wawe radhi kuweka mifumo imara ya kumwezesha kila mmoja kupata
haki kwa wakati,” alisisitiza Mtatiro.
0 comments:
Post a Comment