Breaking News

Saturday

NEYMAR, JORDI ALBA WAFANYIWA UPASUAJI.

NYOTA wa Barcelona, Neymar na Jordi Alba wamefanyiwa kimafanikio upasuaji mdogo wa koo kwa ajili ya kuondoa tonsils jana, klabu hiyo ya Catalunya imethibitisha.Upasuaji huo ulipangwa na Barca kwa matumaini ya kumaliza tatizo hilo linalojirudia baina ya wawili hao.
Klabu hiyo ilisema upasuaji ulienda vyema kama ulivyopangwa na kubainisha kwamba watakuwa nje ya mchezo kwa siku chache sana."Ijumaa hii, Neymar na Jordi Alba wamefanyiwa kimafanikio upasuaji wa matatizo yao ya 'tonsillitis', ambayo yalikuwa yakijirudia katika wiki za karibuni," klabu ilibainisha katika tovuti yake."Muda wa kupona kwa wachezaji wote wawili ni kati ya siku 10."
Wachezaji hao walilazimika kusubiri hadi kumalizika kwa michuano ya Kombe la Mabingwa wa Mabara - ambalo timu ya Neymar ya Brazil iliifunga ya Jordi.Alba ya Hispania 3-0 katika fainali - kabla ya kwenda kufanyiwa upasuaji huo.
**ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU**

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Chapisho Lililoangaziwa

WEDDING PARTY PHILLIPO AND LUSIO

PHILLIPO & LUSIO WEDDING PARTY: STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING MC & MUSIC BY MC SIMBA COMPANY 0715 501 059 ...

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

67153
Powered by Blogger.

Pages