Barca haijaweka wazi taarifa za makubaliano ya fedha za udhamini huo, ambao utakwenda hadi Julai 2016, lakini imeelezewa wateja wa UAB watakuwa wanazawadiwa "siti za vibosile" kuangalia mechi za klabu hiyo.
"Benki ya Umoja wa Arabuni inatazamia kuwapa faraja wateja wake wapendano soka na FC Barcelona kwa ujumla," Barca imesema katika taarifa yake kwenye tovuti yake (www.fcbarcelona.es)."Kama wadhamini rasmi wa klabu, itautumia uhusiano huu na Barca kuwa na bidhaa ambazo zitawafurahisha mashabiki wengi wa Barca UAE."Benki ya Umoja wa Arabuni (UAB), ni taasisi ya kifedha inayokuwa kwa kasi UAE, na imetangaza kuungia ushirika na moja ya klabu kubwa duniani, FC Barcelona.
0 comments:
Post a Comment