Breaking News

Thursday

HABARI NJEMA MAN UNITED, ROONEY AREJEA KAZINI..AANZA MAZOEZI RASMI, NA FELLAINI...

MSHAMBULIAJI Wayne Rooney yuko tayari kuanza mazoezi kamili na Manchester United akidhamiria kuwa kujiweka fiti kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu, City Jumapili.
Rooney, mwenye umri wa miaka 27, alikuwa akifanya mazoezi na wataalamu wa tiba wa United kwenye Uwanja wa mazoezi wa klabu, Carrington jana na anaonekana kuwa fiti baada ya kuumia kichwa alipogongana na Phil Jones kiasi cha wiki mbili zilizopita.
Lakini mshambuliaji huyo United anapewea asilimia 50 kwa 50 kucheza mechi dhidi ya timu ya Manuel Pellegrini, City Uwanja wa Etihad, Septemba 22.

 Wayne Rooney akipiga picha na shabiki baada ya kupona maumivu ya kichwa na kuanza mazoezi jana
Wayne Rooney' alivyoumia kichwani kiasi cha kushindwa kuitumikia England, ila sasa amerejea mazoezini

 Rooney inafahamika alikuwa anafanya mazoezi kivyake nje ya timu, na David Moyes hayuko tayari kumharakisha kurejea uwanjani
Moyes tayari amekubali kumkosa Rooney katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Crystal Palace Ligi Kuu ya England na anatarajiwa kucheza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayer Leverkusen Uwanja wa Old Trafford JUmanne ijayo.
Mchezaji mkubwa pekee aliyesainiwa United ni Marouane Fellaini, mwenye umri wa miaka 25, na anatarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa wiki hii.
Mshambuliaji huyo amecheza kikamilifu mechi moja tu United msimu huu, na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika sare ya 0-0 na Chelsea Uwanja wa Old Trafford. 
Alitokea benchi katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Swansea, akitoa mchango wa kupatikana mabao mawili kati ya manne ambayo timu yake ilivuna siku hiyo.
 Marouane Fellaini amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza United na anatarajiwa kuanza kazi
Rooney anaweza kurejea katika mechi dhidi ya wapinzani wa Jiji la Manchester, Septemba 22

Share:

0 comments:

Post a Comment

Chapisho Lililoangaziwa

WEDDING PARTY PHILLIPO AND LUSIO

PHILLIPO & LUSIO WEDDING PARTY: STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING MC & MUSIC BY MC SIMBA COMPANY 0715 501 059

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Powered by Blogger.

Pages