BAO la penalti dakika za majeruhi la Robin van Persie limeiwezesha Uholanzi kudumisha rekodi ya kutofungwa katika mechi za kuwania tiketi ya Komba la Dunia mwakani Brazil, baada ya kutoa sare ya 2-2 na Estonia.
Uholanzi ambayo ilisafiri hadi Tallinn ikiwa na rekodi ya asilimia 100 katika Kundi D, ilitangulia kupata bao kupitia kwa Arjen Robben na Konstantin Vassiljev akawasawazishia wenyeji.
Wakati dakika zinayoyoma kikosi cha Louis van Gaal kikiwa nyuma kwa 2-1, Van Persie aliinusuru timu yake kuzama katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kuchezewa rafu na Raio Piiroja.
Robin van Persie akiifungia bao la kusawazisha Uholanzi
Uholanzi inaendelea kuongoza kwa pointi sita zaidi, lakini Romania imepaa nafasi ya pili kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Hungary mjini Bucharest.Ciprian Marica alifunga la kwanza dakika ya pili na Mihai Pintilii akafunga la pili na Cristian Tanase akakamilisha hesabu baadaye.Turkey imeitandika Andorra 5-0 katika mechi nyingine ya Kundi D huku Umut Bulut akifunga matatu peke yake na mengine yakifungwa na Burak Yilmaz na Arda Turan.Mabingwa watetezi na mabingwa wa Ulaya, Hispania wameendelea kutawala Kundi I baada ya kuifunga Finland wakati Ufaransa ilibanwa na Georgia.Jordi Alba aliifungia Hispania mapema mjini Helsinki kabla ya mshambuliaji wa Manchester City, Alvaro Negredo kukamilisha ushindi dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho.
Mfungaji wa City: Alvaro Negredo ameifungia Hispania bao la pili ikiifunga Finland
Ufaransa ilitoka sare ya bila kufungana mjini Tbilisi na sasa inazidiwa na Hispania kwa pointi tatu.Croatia iliwaachia nafasi Ubelgiji katika Kundi A baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Serbia mjini Belgrade.Mario Mandzukic alitangulia kuifungia Croatia dakika ya 53 lakini Aleksandar Mitrovic akasawazisha dakika 13 baadaye katika mchezo ambao timu zote zilimaliza na wachezaji 10 baada ya Nemanja Matic wa Serbia na Josip Simunic wa Croatia kutolewa kwa kadi nyekundu.Urusi ya Fabio Capello imeifunga Luxembourg 4-1 mjini Kazan.Alexander Kokorin alifunga mawili, likiwemo moja katika dakika 20 za mwanzo, wakati Alexander Kerzhakov na Alexander Samedov pia walifunga. Nahodha Aurelien Joachim aliifungia bao la kufutia machozi Luxembourg
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Mario Mandzukic akishangilia baada ya kuifungia Croatia
Italia iliiacha kwa pointi saba Bulgaria kileleni mwa Kundi B kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya wapinzani wao hao wa karibu mjini Palermo.
Alberto Gilardino alifunga bao pekee dakika ya 38 lililoipa ushindi Italia, ambayo iliwakosa Mario Balotelli, Dani Osvaldo na Riccardo Montolivo wanaotumikia adhabu. Bulgaria wanabaki nafasi ya pili katika Kundi hilo.
Jamhuri ya Czech ilifungwa 2-1 na Armenia huku Gevorg Ghazaryan akiwafungia mapema wageni mjini Prague kabla ya Tomas Rosicky kufunga la pili, baada ya Karlen Mkrtchya kufunga. Armenia bado ina matumaini ya kufuzu.
Denmark imeshinda 2-1 mjini Malta kwa mabao ya Leon Andreasen na Ryan Camilleri aliyejifunga.
Mshambuliaji wa Italia, Alberto Gilardino puts the ball past Bulgaria's goalkeeper Nikolay Mihaylov
0 comments:
Post a Comment