Lorenzo Insigne na Goran Pandev waliwafungia mabao wageni kipindi cha kwanza, katika mchezo huo wa kujiandaa na msimu, Gunners wakionekana kuzidiwa kipindi cha kwanza.
Hata hivyo, The Gunners walizinduka na kufanikiwa kusawazisha mabao yote, moja la Olivier Giroud kwa tika tak dakika ya 71 na lingine Laurent Koscielny kwa kichwa dakika ya 85, baada ya Insigne kufunga dakika ya saba na Pandev dakika ya 29.
Arsenal walipata nafasi ya kufunga bao la tatu, lakini mkwaju wa penalti wa Lukas Podolski uliokolewa na kipa Pepe Reina wa Napoli.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Fabianski; Jenkinson/Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey, Wilshere, Gnabry/Walcott, Rosicky, Podolski na Giroud.
Napoli: Reina; Mesto, Cannavaro, Britos, Armero, Behrami, Inler, Hamsik, Insigne, Callejon/Maggio, Pandev/Higuain.
Arsene Wenger (kulia) akisalimiana na Rafael Benitez (kushoto) kabla ya mechi yao iliyoisha kwa 2-2
Bao la kwanza: Lorenzo Insigne akishangilia bao la kwanza aliloifungia Napoli
Wachezaji wakiwa wamemzingira refa baada ya Arsenal kupewa penalti, ambayo iliokolewa na Pepe Reina (wa pili kushoto) baada ya Lukas Podolski kupiga.
Goran Pandev alifunga la pili kwa Napoli
Giroud aliifungia Arsenal kwa tik tak
Gonzalo Higuain akikabiliana na Laurent Koscielny
0 comments:
Post a Comment