Breaking News

Saturday

KIASI CHA MSAADA WA SH1.5 MILIONI INAHITAJIKA KWA AJILI YA MATIBABU YA KANSA YA NGOZI KUMTIBU MTOTO ASHURA.


MTOTO Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani  Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.   

Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema kuwa mtoto wake anateseka na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na umri wa mwaka mmoja.


Makombe alisema kuwa ugonjwa huo ulianza kama malengelenge akiwa na umri huo na wakawa wanaenda hospitali ndogo ndogo lakini baadaye wakaamua kumpeleka hospitali ya furaa ya Muhimbili ambapo walipewa barua yenye maelekezo kwenda hospitali ya CCBRT ambako ndiko walikogundua kuwa mtoto wake ana kansa ya ngozi hatua ya nne.



“Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.


“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. 


Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 na 0715 424697 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema Makombe.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Chapisho Lililoangaziwa

WEDDING PARTY PHILLIPO AND LUSIO

PHILLIPO & LUSIO WEDDING PARTY: STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING MC & MUSIC BY MC SIMBA COMPANY 0715 501 059

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Powered by Blogger.

Pages