Pamoja na habari za Luis Suarez kuondoka kuwa ajenda kuu kwa sasa, kikosi cha Brendan Rodgers leo kimeifumua valeranga mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Ullevaal, mjini Oslo, Norway katika mchezo wa kirafiki.
Shukrani kwao wafungaji wa mabao ya leo, Luis Alberto, Iago Aspas, Martin Kelly na Raheem Sterling katika mchezo wa leo, Liverpool ikishuhudiwa na mmiliki wake, John W Henry kwa mara ya kwanza baada ya miezi 13 ikiweka rekodi ya kushinda mechi ya sita.
Alberto alifunga dakika ya 31, Aspas dakika ya 42, Kelly dakika ya 54 na Sterling dakika ya 90, wakati bao la wenyeji lilifungwa na Giancarlo Gonzalez dakika ya 35.
Kikosi cha Liverpool leo kilikuwa: Jones/Mignolet dk46, Alberto/Coutinho dk46, Aspas/Borini dk46, Henderson/Gerrard dk46, Coates/Toure dk46, Downing/Sterling dk46, Spearing/Kelly dk46, Allen/Lucas dk46, Flanagan/Enrique dk46, Ibe/Assaidi dk46 na Wisdom.
Valerenga: Kongshavn/Knutsen dk85, Larsen/Wawrzynkiewicz dk51, Gonzalez, Hogh, Lecjaks, Ogude/Nasberg dk62, Zajic/Haested dk57, Holm/Zahid dk57, Fellah, Berre/Borven dk67 na Calvo.
Iago Aspas akiifungia Liverpool kabla ya mapumziko
Mashabiki wa Liverpool mjini Oslo wakionyesha kumuunga mkono kocha Brendan Rodgers na timu yake
Gwiji wa Liverpool, Ian Rush akifanyiwa mahojiano wakati wa mapumziko
0 comments:
Post a Comment