The Gunners imemuweka nambari moja mshambuliaji huyo anayetaka kuondoka Liverpool, lakini tayari ofa zao mbili zimekwishapigwa chini na klabu ya Anfield.
Arsenal bado ina matumaini ya kushinda sakata hilo kwa kumnsa mpachika mabao huyo tishio, ikibidi kutuma ofa ya tatu ya Pauni Milioni 50, kiwango cha chini kinachotakiwa na Liverpool.
Niagalie: Luis Suarez anafanya mazoezi peke yake Melwood kama adhabu baada ya kulazimisha kuondoka
Kupitia sports inafahamu kwamba The Gunners imeanza mpango wa kumpata mkali mwingine, iwapo itamkosa Suarez.Majadiliano baina ya benchi la Ufundi na Maskauti wa klabu yamechukua nafasi siku chache zilizopita juu ya mchezaji mbadala.
Tayari, Arsenal imewakosa Gonzalo Higuain na Stevan Jovetic ambao wote kocha Arsene Wenger alikuwa anawahitaji sana majira haya ya joto, hivyo akahamia kwa Suarez.
Anatakiwa? Edin Dzeko, pichani mjini Munich akiwa na Manchester City, amerudi katika kiwango kwenye mechi za kujiandaa na msimu
Wengine wanaotakiwa: Stevan Jovetic (kulia) amechagua Manchester City, lakini Michu (kushoto) anabaki kwenye rada za Arsenal
Mmoja aliyeota mbawa: Gonzalo Higuain (katikati) ametimkia Napoli. Hapa akishangilia kufunga dhidi ya Benfica
Higuain ameenda Napoli na Jovetic ametua Manchester City, wakiiacha The Gunners ikisotea sani za wengine.
Wayne Rooney alikuwa anatakiwa pia mwanzoni, wakati klabu hiyo imepokea taarifa ya Maskauti wake kuhusu mshambuliaji wa Swansea, Michu na wa Manchester City, Edin Dzeko.
Liverpool wanasistiza hawatamuuza Suarez kwa Arsenal kwa namna yoyote, lakini The Gunners haijabwaga manyanga katika jaribio lake la kunasa saini ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay, ambaye yu tayari kuondoka Anfield kutua Emirates.
Mchezaji pekee ambaye Arsenal ipo kwenye nafasi nzuri ya kumsajili ni kiungo mkabajia wa Bayern Munich, Luis Gustavo.
The Gunners imeanza mazungumzo na mabingwa hao wa Ulaya juu ya ofa ya Pauni Milioni 14.5 kumnasa mwanasoka huyo wa kimataifa wa Brazil.
Bado anasaka: Arsene Wenger (kulia), akizungumza na Manuel Pellegrini, anataka kuongeza wachezaji kikosini mwake
"Nataka kwenda klabu ambayo nitacheza,". Wakati huo huo, Malaga inataka kumtumia beki wa kulia, Jesus Gamez kama sehemu ya majadiliano ya kumsaini Nicklas Bendtner.
Arsenal inataka kusaini beki mpya wa kulia awe msaidizi wa Bacary Sagna, ambaye anaweza kutumika katika beki ya kati mwanzoni mwa msimu kutokana na Thomas Vermaelen kuwa majeruhi.
Na Malaga inataka kumtumia Gamez, mwenye umri wa miaka 28, kama sehemu ya dili lao na Gunners kwa Bendtner.
Anayetoka na Anayeingia: Luiz Gustavo (kushoto) anaweza kutua akitokea Bayern Munich wakati Nicklas Bendtner anataka kuondka
0 comments:
Post a Comment