Breaking News

Thursday

HUYU NDIYE BINTI RAIA WA NCHI YA NIGERIA, ANTHONIA OJO ALIYEANASWA NA KETE 99 ZA DAWA ZA KULEVYA.



 Anthonia Ojo (25) Raia wa Nigeria akiwa na kete 99 za madawa ya kulevya baada ya kukamatwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam jana, akieleke Roma Italia kupitia Paris Ufaransa kwa ndege ya Ethiopian Airways. 
Msichana huyo aliingia hapa nchini Agosti 30 akitokea Nigeria. Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege, Renatus Chalya, Ojo anaendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwa ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo, thamani yake na hatimaye atafikisha mahakamani.
SEHEMU YA KETE 99 ALIZOKAMATWA NAZO. 
Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu dk. harisson mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini nigeria anthonia ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya dar es salaam jana.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Chapisho Lililoangaziwa

WEDDING PARTY PHILLIPO AND LUSIO

PHILLIPO & LUSIO WEDDING PARTY: STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING MC & MUSIC BY MC SIMBA COMPANY 0715 501 059

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Powered by Blogger.

Pages