Breaking News

Wednesday

MAPIGANO KATI YA WANAOMUUNGA MKOANO RAIS FRANCOIS BOZIZE NA WAASI WANAOSHIKILIA MADARAKA YASABABISHA RAIA 60 KUPOTEZA MAISHA.

SERIKALI ya Jamhuri ya Afrika ya Kati inasema watu 60 wameuwawa katika mapigano kati ya wapiganaji wanaomuunga mkono rais aliyetimuliwa madar
akani Francois Bozize na waasi wanaoshikilia madaraka.
Msemaji wa serikali Guy Simplice Kodegue anasema mapigano hayo yalitokea Jumamosi na Jumapili katika mji wa kaskazini magharibi wa Bossangoa nyumbani kwa Bw. Bozize.
Umoja wa Mataifa unasema asilimia 80 ya watu wa mji huo  ambao wanakisiwa kuwa 30,000 wamekimbilia porini na maeneo mengine.
 Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema wafanyakazi wake wawili ni miongoni mwa waliouawa katika ghasia hizo.
Mapigano hayo  yalikuwa kati ya  makundi ya wanamgambo na  kundi mseto la waasi wa Seleka ambao walihitimisha utawala wa miaka 10 wa rais Bozize mwezi Machi . Kundi hilo la Seleka linajaribu kufanya mabadiliko ya kisiasa ili kuandaa uchaguzi mkuu wa kitaifa katika muda wa miezi 18 ijayo.  
Kufikia sasa Umoja wa Mataifa unasema ghasia katika taifa hilo zimesababisha wananchi wapatao 62,000 kutafuta hifadhi nje ya nchi tangu mwanzo wa mwezi huu wa Septemba.
 Jamhuri ya Afrika ya Kati imekumbwa na msururu wa mapinduzi ya serikali na maasi  tangu ilipopata uhuru wake kutoka Ufaransa mwaka wa Source:
www.voaswahili.com
Share:

0 comments:

Post a Comment

Chapisho Lililoangaziwa

WEDDING PARTY PHILLIPO AND LUSIO

PHILLIPO & LUSIO WEDDING PARTY: STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING MC & MUSIC BY MC SIMBA COMPANY 0715 501 059

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Powered by Blogger.

Pages