
TAARIFA KWA UMMA
KUONGEZWA KWA
MUDA WA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014
Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza,
Wanafunzi wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kuwa muda wa maombi ya
mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja hadi Julai 31, 2013.
Pamoja na nyongeza
hii ya muda, Bodi inasisitiza waombaji kujaza fomu za maombi ya kwa njia ya
mtandao (OLAS) kwa usahihi na kuzingatia muda wa maombi uliowekwa ili kuepuka
usumbufu usio wa lazima. Waombaji wa mara yakwanza wahakikishe
wanajaza kwa ufasaha na kuweka viambatanisho vyote muhimu ili kufanikisha
mchakato wa uchambuzi na upangaji wa mikopo.
Kundi la kwanza la
wanafunzi waliopangwa kulitumikia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambao wamemaliza
mafunzo hayo mwezi Juni, 2013 wanapaswa kutumia fursa hii kujaza fomu za maombi
ya mikopo bila kukosa. Aidha, kundi la pili la wanafunzi wanaotegemea kuanza
mafunzo hayo mwezi Julai, 2013 walitakiwa wawe wameshaomba mikopo kati ya
tarehe 1 Mei, 2013 na 30 Juni, 2013 lakini endapo kuna wachache ambao
hawakuweza kufanya hivyo basi nao watumie muda huu wa nyongeza kujaza fomu za
maombi kwa njia ya mtandao wakiwa huko huko JKT.
Endapo mwombaji
yeyote atakabiliana na matatizo wakati wa kujaza fomu yake anashauriwa kupiga
simu kwenye dawati la huduma kwa wateja kwa namba 022 550 7910 kati ya saa 2.00
asubuhi na saa 2.00 usiku siku za Jumatatu hadi Ijumaa, na kati ya saa 2.00
asubuhi na saa 10.00 jioni siku za Jumamosi.
Ikumbukwe kwamba
Bodi haitaongeza muda wa ziada baada ya Julai 31, 2013 ili kutoa nafasi kwa
Bodi kuendelea na mchakato wa uchambuzi na upangaji mikopo.
IMETOLEWA NA:
BODI YA WAKURUGENZI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA
JUU.
*ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU*
0 comments:
Post a Comment