Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman ameweka bayana kuwa wanaunga mkono Rasimu ya Katiba na hasa suala la
Muungano wa Tanzania kuundwa na Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba.
Amesema mambo mengi yaliyopendekezwa na chama chake yamefanyiwa
kazi na Tume ya Mabadiliko na kuishangaa CCM akidai kwamba inapinga rasimu hiyo
hususan suala la Serikali tatu wakati kimsingi watu wa Tanzania Bara wamekuwa
wakipunjika kwenye muundo wa sasa wa Muungano.Akihutubia mkutano wa kampeni ya
kuwania udiwani wa Kata ya Iyela katika Uwanja wa Bongonela, Mbeya jana jioni,
Mbowe alisema chama chake kinataka kuona Serikali ya Tanganyika ikifufuliwa.
Alikuwa akimnadi mgombea wa Chadema, Charles Mkela.
Alisema Chadema kinataka kuona Wazanzibari wakiwa na Serikali
yao ili wajiamulie mambo yao na pia Watanganyika wawe na uongozi wao lakini
waunganishwe na Serikali ya Muungano.
Alisema muundo wa sasa wa Muungano una matatizo. Kwa mfano,
mbunge wa Zanzibar anawakilisha watu wachache zaidi ukilinganisha na mbunge wa
Bara. Wananchi mtashangaa sote tunalipwa sawa.”
“Ila zikija Serikali tatu ina maana kuwa kila upande wa Muungano
utatumia rasilimali zake. Haya mambo kulipana fedha nyingi kwa kazi kidogo
yatakoma.”
Msimamo wa Sumaye
Sumaye alisema muungano wa Serikali tatu haufai akisema
utasababisha mvutano mkubwa wa kimadaraka na rasilimali.Sumaye anaungana na
wanasiasa wengine waliopinga muundo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba wengine wakiwa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Samuel Sitta, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene, Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM) Profesa Juma Kapuya, Mbunge wa
Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba na Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano na
Uchukuzi, Dk Maua Daftari.
Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha Dira ya Dunia
kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), akiwa Johannesburg,
Afrika Kusini mwishoni mwa wiki, alisema Serikali tatu zinaweza kutikisa
Muungano.
“Huwezi kutatua matatizo kwa Serikali tatu... unaweza kuyaongeza
kwani kutakuwa na Serikali tatu na marais watatu... kama kuna mvutano baina ya
Serikali mbili ukiongeza ya tatu inaweza kuwa na mvutano zaidi,” alisema na
kuongeza:
Profesa Lipumba alisema hakuna mantiki ya kupiga kura ya maoni
ya Katiba ya Muungano bila kuwa na Katiba ya Tanzania Bara na marekebisho ya
Katiba ya Zanzibar.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
Profesa Lipumba alisema mapendekezo ya msingi ya CUF ni kwamba, kura ya maoni
isubiri kukamilishwa kwa rasimu ya Katiba ya Tanzania Bara na marekebisho ya
Katiba ya Zanzibar.
Alisema licha ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kufanya kazi nzuri
ya kuratibu maoni bila kushinikizwa na matakwa ya CCM, kuna baadhi ya mambo ya
msingi ambayo yameachwa kwenye rasimu.“Huwezi kuacha vitu kama umilikaji wa
ardhi, maliasili na rasilimali za nchi, elimu, afya na mazingira ya kukuza
uchumi na uhuru wa Serikali za mitaa. Rasimu imeshughulikia mambo ya Muungano.”
“Maoni ambayo CUF tuliyatoa ikiwamo muundo wa Serikali tatu,
kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, Rais kutangazwa baada ya kushinda kwa zaidi ya
asilimia 50 ya kura zote, Spika kutokuwa mbunge na mengineyo yamepata nafasi.” Imeandikwa na Brandy Nelson,
Ibrahim Yamola na Aidan Mhando.
*ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU*







0 comments:
Post a Comment