Mbunge wa jimbo la Mtwara, eneo ambalo limekumbwa na vurugu hivi karibuni
kusini mwa Tanzania amefikishwa mahakamani akituhumiwa kwa makosa ya
uchochezi wa vurugu zilizo sababisha vifo vya watu watatu mwezi uliopita.
Hasnain Murji
pamoja na watuhumiwa wengine 91 wamefikishwa kwenye mahakama ya wilaya ya
Mtwara.
Kwa muda huu
baadhi ya watuhumiwa wamepata dhamana huku wengine wakiendelea na taratibu za
kukamilisha udhamini, wakati Mbunge huyo akisubiri kupandishwa kizimbani na
kusomewa mashtaka yanayo mkabili.
Wananchi waliofika
mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi zinazowakabili ndugu na jamaa zao
wamelalamikia utaratibu wa kuwazuwia kuingia mahakamani hapo.
Mbunge huyo wa
Chama kinacho tawala nchini humo CCM, alikamatwa na kushikiliwa na jeshi la
Polisi mkoani humo siku ya Jumamosi.
Idadi kubwa ya
wananchi wa Mtwara wamekuwa katika mvutano mkali na Serikali yao ambayo
imekusudia kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia inayopatikana mkoani humo
hadi Dar es Salaam, Hatua inayopingwa na wananchi hao ambao wanadai gesi hiyo
isisafirishwe na kupelekwa popote.
*ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU*
0 comments:
Post a Comment