Usiku wa jana ulikuwa ni usiku wa furaha sana kwa Mashujaa
Band ambao waliongoza kwa kuondoka na tuzo nyingi kuliko wasanii wengne.
Mashujaa ambao wanafanya vizuri na wimbo wao wa ''Kidole Risasi'' waliondoka na
kura 5 ikiwa ni pamoja na msanii bora wa kiume band Charz Baba, mtunzi bora a
mashari ya band Charz Baba, rapper bora wa band Furguson, wimbo bora wa band
Risasi Kidole na tuzo ya tano waliichukuwa kupitia category ya band bora ya
mwaka huku wakiwatupa kule Twanga Pepeta, Mapacha Watatu na Msondo
Ngoma
Wakati huo, upande wa hiphop, Kala Jeremiah aliondoka na tuzo tatu na kuwaacha chini akina Fid Q,Stamina na wengineo, ambapo aliondoka na tuzo ya msanii bora wa hiphop, mtunzi bora wa mashairi ya hiphop na wimbo bora wa mwaka ''Dear God''Kala ambae ni mwenyeji wa mwanza ambae alikiri kuwa hiyo ilikuwa kama miujiza kwakwe kuweza kutwaa tuzo zote hizo kwa mpigo
Ommy Dimpoz nae, alisepa na tuzo tatu , wimbo bora wa kushirikiana ''me and you'', video bora ya mwaka ''Baadae'' na wimbo bora wa bongo pop
Mrisho Mpoto ameondoka na tuzo ya wimbo bora wenye vionjo vya asili ''chocheeni kuni''
Ben
pol aliondoka na tuzo ya mtunzi bora wa muziki bongo fleva
wengine
ni pamoja na Diamond ambae aliondoka na tuzo ya msanii bora wa kiume na
msanii bora wa kiumee bongo fleva. msanii anaechipukia ''Ally Nipishe'',
mtayarishaji anaechipukia ''Mensen Selector, wimbo bora wa hiphop ''nasema
nao'' Ney wa mitego, wimbo bora wa Zouk/Rhumba ''ni wewe'' Amini, wimbo bora wa
Africa mashariki ''Valu valu'' Chameleon, msanii bora wa kike ''Jay Dee,
*ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU*
0 comments:
Post a Comment