Waziri wa Mambo ya Nje,
Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati
wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika
jiji hilo.
Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali
duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership
utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika
maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa
upekuzi kwa wageni wake.
“Hoteli na nyumba za
wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za
kijamii zitakuwa shida,” alisema.
Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na
tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili.
Mbali ya ujio huo,
wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa
Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo
utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.
“Jiji la Dar es
Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute
safari zao,” alisema na kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na
hawana sababu za kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu
jiji la litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni
hao.”
Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya
barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine
zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na ile ya Mwai Kibaki
na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda
Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi
Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme
ya Kampuni ya Symbion Ubungo.
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo
inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa 4.00
asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa mizigo na
abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia kwakupitia barabara ya morogoro
road
*ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU*
0 comments:
Post a Comment