Breaking News

Sunday

TUKIO ZIMA LA MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI ZA UDIWANI CHADEMA SOWEPO JIJINI ARUSHA.

Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na kinacho semekana kuwa ni mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hosp

itali ya Seliani na Mount Meru.mlipuko huo unasemekana kuwa ulitokea kwenye mkusanyiko wa watu, mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.

Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.

Polisi wapo katika eneo hilo la tukio wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA.
 


VIONGOZI WA CHADEMA WAKITUA KATIKA UWANJA TAYARI KUANZA MKUTANO
 UMATI WA WATU WALIO HUDHURIA MKUTANO HUO HAPO JANA

BAADHI YA PICHA ZA MAJERUHI KATIKA TKIO HILO INASIKITISHA SANA.









Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Chapisho Lililoangaziwa

WEDDING PARTY PHILLIPO AND LUSIO

PHILLIPO & LUSIO WEDDING PARTY: STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING MC & MUSIC BY MC SIMBA COMPANY 0715 501 059 ...

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

67154
Powered by Blogger.

Pages