TUKIO la ugaidi iliyotokea katika mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesababisha vifo vya watu wawili na kujerugi watu 11,tukio hilo la kigaidi lilitokea wakati Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wakiwa katika hat ua za mwisho za kufunga mkutano huo. Akizungumza na mwandishi wetu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema amepokea maiti moja ya mtoto na majeruhi 11, Wakati Mganga huyo akieleza kuwa amepokea maiti moja ya mtoto, Mwandishi alishuhudia zaidi ya majeruhi saba katika Hospitali ya Misheni ya Selian, huku pia ikidaiwa kwamba kuna maiti za watu watatu katika Hospitali hiyo. Akizungumzia tukio hilo la ugaidi iliyotokea katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili mwanamke na mwanamume wamepoteza maisha, huku akidai kwamba bado wanafuatlia idadi ya majeruhi waliotawanywa katika Hospitali mbalimbali mkoani humo. Mashuhuda wa tukio walipozunguza na Mwandishi aliyekuwa katika mkutano huo jana walisema kwamba kuna mtu alionekana akirusha kitu kilichodhaniwa kuwa ni bomu,kabla ajakamatwa Askari wa Jeshi la Pollisi waliokuwa wakilinda mkutano huo wakaanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya machozi na kupiga risasi za moto. Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu wengi mkoani humo, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.
*ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU*
0 comments:
Post a Comment