Timu
ya Taifa ya Soka ya Uganda, imeilaza Liberia kwa bao moja kwa bila na
kuimarisha matumaini yake ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini
Brazil, katika mechi kali iliyochezwa mjini Kampala.
Kufuatia
ushindi huo Uganda Cranes sasa imepanda hadi nafasi ya pili katika kundi J na
alama 5 nyuma ya vinara wa kundi hilo Senegal ambao wanachuana na Angola.
Uganda
sasa imesalia na mechi mechi mbili na imepangiwa kuchuana na Angola tarehe 15
mwezi huu kabla ya kupepetana na Senegal tarehe 6 Septemba mwaka huu katika
uwanja wa Leopold Senghor.
Uganda
ni sharti ishindi mechi zake zilizosalia ili kuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu
kwa fainali hizo zitakazoandaliwa nchini Brazil Januari mwakani.
Katika
mechi zingine za kufuzu kwa Fainali hizo, Zambia wameilaza Lesotho kwa magoli
4-0 nayo Botswana wakalemewe nyumbani kwao na Ethiopia kwa kufungwa magoli 2-1
0 comments:
Post a Comment