Breaking News

Sunday

BASI LA KAMPUNI YA SUMRY LILILOTUMBUKIA MTONI NA KUUA WATU TISA KATIKA KIJIJI CHA SITALIKE MKOA WA KATAVI.



BASI la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni Iku na kuuwa watu tisa na kujeruhi wengine hamsini na tatu katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T 909 AZT mali ya kampuni ya Sumry
lililokuwa likiendesha na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa  jina la Ntungu.
Alisema basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko dereva wake alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza kutoka na kukimbilia kusikojulikana .
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole wahanga wa ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Chapisho Lililoangaziwa

WEDDING PARTY PHILLIPO AND LUSIO

PHILLIPO & LUSIO WEDDING PARTY: STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING MC & MUSIC BY MC SIMBA COMPANY 0715 501 059 ...

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

67153
Powered by Blogger.

Pages