![]() |
Alvaro Negredo |
![]() |
Alvaro Negredo |
MSHAMBULIAJI Alvaro Negredo anatarajiwa kukamilisha uhamisho
wake wa Pauni Milioni 20 kutua Manchester City wiki hii.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 wa Sevilla, ambaye
alikaribia kujiunga na Atletico Madrid, lakini nia ya kuchezea timu inayofundishwa
na Manuel Pellegrini, City imeelezwa kumfanya abadili njia na sasa anakuja
KLigi Kuu ya England.
![]() |
MANUEL PELLEGRINI |
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Hispania, alimaliza wa nne katika
ufungaji bora wa La Liga msimu uliopita kwa mabao yake 25 katika ligi hiyo,
alitaka kusajiliwa na Pellegrini wakati alipokuwa Malaga, lakini dili hilo
halikufanikiwa.
City inataka kuboresha safu yake ya ushambuliaji baada ya
kuwauza Mario Balotelli kwenda AC Milan Januari mwaka huu na Carlos Tevez
kwenda Juventus mwezi uliopita.
Klabu hiyo ilikuwa inamtaka mshambuliaji wa Napoli, Edinson
Cavani, ambaye yuko mbioni kutua Paris St Germain kwa Pauni Milioni 50, dau
ambalo limemkatisha tamaa Pellegrini na sasa anaelekeza nguvu zake kwa Negredo,
aliyeanzia soka katika kikosi cha wachezaji wa akiba wa Real Madrid, akiamini
atafanya vizuri City
Atletico Madrid inaweza kuhamia kwa Edin Dzeko ikiwa watampoteza
kwa City, Negredo, mchezaji wa zamani wa mchezaji mpya aliyesajiliwa
majira haya joto, Jesus Navas.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Bosnia, Dzeko amekuwa pia
akihuishwa na mpango wa kuhamia Napoli kama mbadala wa Edinson Cavani anayeweza
kutua PSG kwa Pauni Milioni 53.However, Rafa Benitez is considering other
targets.
Pellegrini atafurahi Dzeko akibaki City, lakini mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 27 anataka kucheza na kuuzwa kwake, kutatoa nafasi kwa
wengine kama Negredo na beki wa Real Madrid, Pepe.
0 comments:
Post a Comment