“Najua
Kaseja ameachwa Simba SC, na nasikia watu wanamzungumzia sana wakimhusisha na
Azam. Mimi nakubali yule ni kipa mzuri na ana uzoefu. Ila mimi nina makipa
wazuri wawili, Aishi na Mwadini. Nataka hawa wagombee kuwa kipa wa kwanza wa
timu,”alisema.
Hall amesema kwamba bado Azam ina makipa wengine wazuri wa timu za vijana, ambao watakuwa wakipewa nafasi ya kujifua na kikosi cha kwanza msimu ujao.
“Kama nitakuwa na Aishi na Mwadini kama makipa wawili imara wa timu ya kwanza, maana yake Wandwi ataendelea kuua kiwango chake. Nimeona bora nimpeleke Ashanti ili akakusanye uzoefu, baadaye arejee kwenye timu akiwa imara,”alisema

Aidha,
kuhusu maandalizi ya msimu mpya, Hall amesema kwamba kwa sasa Azam ambayo
itaiwakilisha Tanzania kwa mara ya pili mfululizo kwenye Kombe la Shirikisho
Afrika mwakani, iko katika mazoezi.
“Tunaendelea na mazoezi ya msimu mpya. Kwa sasa tupo katika programu ya ufukweni na gym. Baada ya hapo tutaanza programu rasmi ya uwanjani. Lakini wiki mbili za mwanzo za Agosti tutakwenda Afrika Kusini kuweka kambi,”.
“Tukiwa huko tutafanya mazoezi katika Uwanja mzuri na kupata mechi nne za kujipima nguvu dhidi ya timu kama Orlando Pirates, Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundwons na nyingine,”alisema

0 comments:
Post a Comment