Jaji mkuu wa mahakama ya juu zaidi ya
kikatiba ameapishwa nchini Misri kuwa rais wa muda baada ya jeshi kumng'oa
mamlakani rais aliyechaguliwa na raia kwa njia ya kidemokrasia na kushinda kwa
wingi wa kura, Mohammed Morsi. Vingozi wa kimataifa wameelezea wasiwasi kuhusu kuhusu hatua
ya kumpindua mamlakani rais huyo.
Mkuu wa jeshi Generali Abdul Fattah
al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika kile
Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi. Generali Sisi alisema kuwa Morsi,ambaye ni rais wa kwanza
kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu. Hatua hiyo inakuja baada ya siku nyingi ya maandamano, dhidi
ya rais Morsi wa chama cha Musolim Brotherhood. Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa kusukuma
ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi
yanayokumba taifa hilo.Chama cha Muslim Brotherhood
kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha
nyumbani na hawana mawasiliano ya nje. Hapo awali mkuu wa majeshi alisema kuwa katiba ya nchi hiyo
imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa mamlaka ya rais. Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi mjini Cairo
walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo ya jeshi lakini wale
wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana kubaki kimya huku wakisubiri matukio
yatakayofwata.Rais Obama amesema kuwa ana
wasiwasi mkubwa kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa
umoja wa mataifa Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.
0 comments:
Post a Comment