Anaitwa Shilole na Skwadi lake wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013
Pichani ni sehemu ya wakazi wa Mkoa Iringa na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 linaloendelea kufanyika hivi sasa katika uwanja wa Samora.
Mmoja wa Wasanii mahiri katika anga ya muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye uwanja wa Samora,ambapo tamasha la Serengeti fiesta linafanyika usiku huu.
Moja ya kikundi mahiri kutoka jijini Dar,chenye maskani yake Kinondoni,KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza moja ya wimbo wa Michael Jackson,mbele ya wakazi wa Iringa wakati tamasha la Serengeti fiesta likiendelea usiku huu ndani ya uwanja wa Samora.
Msanii aliyewahi kuiwakilisha vyema shindano la BSS,Walter Chilambo akiimba jukwaani usiku huu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kwenye uwanja wa Samora.
Mmoja ya wasanii wa kike wanaokuja kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Bongofleva,Neylee akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Samora.
Mzee wa mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Wasanii wanaokuja juu katika anga ya muziki wa kizazi kipya-hip hop.Stamina na Young Killer wakilishambulia jukwaa kwa pamoja huku mayowe yakiwa yametawala kila kona ya uwanja.
Anajiita Rais wa Manzese,kutoka kundi la Tip Top Connections,Madee akiwaimbisha mashabiki wake wimbo wa Nani kaiba yangu usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,linalofanyika ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
0 comments:
Post a Comment