Tangawizi ina faida nyingi sana kwa mwili wa mwanadamu. Baadhi ya faida hizo ni kama ifuatavyo :1. Kutibu kutokusagika kwa chakula tumboni,.2. Kutibu tatizo la gesi tumboni3. Kuondoa tatizo la msokoto wa tumbo (bila kuharisha)4. Husaidia kuzuia kutapika.5. Mshtuko/Mkazo wa ghafula (wa msuli),6. Maumivu ya tumbo na Kibofu cha mkojo ikiambatana na Homa, Mafua, Kukohoa na Pumu.
JAM YA TANGAWIZI.Unaweza kutumia Jam ya Tangawizi kujitibu magonjwa mbalimbali kama ilivyo onyeshwa hapo juu. JINSI YA KUTENGENEZA JAM YA TANGAWIZI.
Kamua TANGAWIZI mbichi kisha changanya maji yake (Juice) na Sukari. Chemsha mpaka mchanganyiko huo uwe mzito. Ongeza Zafarani iliyosagwa,Iliki iliyosagwa, Kungumanga zilizosagwa na karafuu iliosagwa. Iweke dawa hii vizuri na tumia inapo hitajika.
MUONGOZO WA KUJITIBU MAGONJWA MBALIMBALI KWA KUTUMIA TANGAWIZI.
Unaweza kujitibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia zao la Tangawizi kwa kufuata maelekezo yafuatayo :
KUJITIBU TATIZO LA KUVIMBIWA NA KUKOSA HAMU YA KULA.
Changanya Juice ya TANGAWIZI, Juice ya Limau na Chumvi Mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya Chakula. Vingineyo changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI na Sukari Mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula chakula. Dawa hii husafisha Ulimi na Koo na hukuongeza hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.
KUJITIBU TATIZO LA MAUMIVU YA KUKOO NA KUKAUKA SAUTI
Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.
KUJITIBU TATIZO LA KUHARISHA.Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa Juice ya Tangawizi.
KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKAKunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi na Juice ya Kitunguu.
MAUMIVU YA KICHWA CHA WASIWASIChanganya Juice ya Tangawizi na Maziwa, kisha kausha. Nusa unga huo kama Tumbaku.
MAUMIVU MAKALI YA TUMBOChanganya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.
BARIDI YABISI SUGUChanganya kijiko kimoja cha Tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huu ukiwa vuguvugu. Ulale na ujifunike mpaka utoe jasho.
KUUMWA JINO NA MAUMIVU YA KICHWAChukua Tangawizi ya Unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu. Kwa maelezo zaidi kuhusu tiba zetu , wasiliana nasi kwa simu 0767010756 au 0766538384
0 comments:
Post a Comment