Breaking News

Thursday

VAN PERSIE AKANA KUMKUMBUKA FERGSUON, ASEMA MOYES POA SANA TU

MSHAMBULIAJI Robin van Persie amepuuza tetesi kwamba hafurahii maisha chini ya kocha mpya Manchester United, David Moyes.
Taarifa za Daily Star na Metro zilisema kwamba van Persie amewaambia rafiki zake anamkumbuka kocha wa zamani wa United, Sir Alex Ferguson, na Mholanzi huyo amesema hashawishiki na ufundishaji wa Moyes.

Van Persie alifurahia matunda katika mechi ya kufungua msimu, akifunga mabao mawili katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Wigan kabla ya kufunga tena mawili katika ushindi wa United wa 4-1 dhidi ya Swansea.

Mholanzi: Robin van Persie (katikati kushoto) ameshindwa kufunga kwenye Ligi Kuu chini ya kocha mpya, David Moyes
 Pamoja na hayo, mshambuliaji huyo alishindwa kufurukuta katika sare ya United ya 0-0 nyumbani dhidi ya Chelsea kipigo cha 1-0 dhidi ya Liverpool.
Van Persie alionekana kuchanganyikiwa na hali ya mambo Anfield, na Mholanzi huyo alilimwa kadi ya njano na angeweza kutolewa nje kwa kadi nyekundu kilaini baada ya kupambana na Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard.
Lakini Van Persie, aliyefunga mabao 30 United msimu uliopita, amesema anafurahia zama mpya Old Trafford.
Mholanzi huyo hakufurahia matokeo dhidi ya Liverpool
Aliliambia De Telegraaf: "Ni babu kubwa kufanya kazi na kocha mpya David Moyes. Ninafurahia mtindo wa Moyes. Anafanyisha mwenyewe mazoezi; yupo karibu na wachezaji na anatuandaa na kutupa maelekezo vizuri kwa mchezo dhidi ya wapinzani wafuatao. Ambayo inatuweka vizuri,".
"Kuna hali nzuri ya kufurahisha katika klabu. Taji la mwaka jana limetupa njaa zaidi ya mataji,"alisema.

Van Persie alikuwa ana bahati kutoonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Gerrard (katikati)
Van Persie naFerguson
Share:

0 comments:

Post a Comment

Chapisho Lililoangaziwa

WEDDING PARTY PHILLIPO AND LUSIO

PHILLIPO & LUSIO WEDDING PARTY: STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING MC & MUSIC BY MC SIMBA COMPANY 0715 501 059

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Powered by Blogger.

Pages