
Kiongozi wa mwisho wa Afrika
Kusini ya ubaguzi wa rangi ambaye pia alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel
sambamba na Nelson Mandela kwa kusaidia kuhitimisha utawala wa weupe wachache
anatarajiwa kupachikiwa kifaa cha kurekebisha mapigo ya moyo baada ya kuugua.
Rais wa zamani Frederic William de Klerk,
mwenye umri wa miaka 77 alijihisi kizunguzungu baada ya kurejea nyumbani kutoka
Ulaya Jumapili iliyopita.
Alikuwa akisumbuliwa na matatizo kadhaa
yanayof
anana na hayo ya kizunguzungu katika wiki za karibuni.
anana na hayo ya kizunguzungu katika wiki za karibuni.
Alitarajiwa kupachikiwa kifaa hicho cha
kurekebisha mapigo ya moyo jana kusaidia moyo wake kufanya kazi na alitarajiwa
kubaki hospitalini hapo usiku huo.
Hili limekuja huku Mandela, mwenye miaka
94, akitimiza siku yake ya 25 hospitalini jana baada ya mwanzoni kuwa amelazwa
kwa kujirudia maambukizi kwenye mapafu yake.
Tangu hapo, kumekuwa na hali ya
sintofahamu nchini Afrika Kusini na duniani kwa ujumla kwa mtu huyo ambaye
alitumikia miaka 27 kama mfungwa chini ya ubaguzi wa rangi na kisha kuibuka
baadaye kujadiliana mwisho wa utawala wa wabaguzi weupe kabla ya kuwa rais.
Akiwa rais, de Klerk alimwachia huru
Mandela kutoka gerezani. de Klerk na kiongozi huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi
kisha wakaongoza majadiliano ambayo yalihitimisha utawala wa wabaguzi weupe.
Yeye na mkewe, Elita hapo kabla
walitangaza kuahirisha ziara ya kikazi na mapumziko barani Ulaya sababu Mandela
anaumwa mahututi.
Taasisi moja yenye makao makuu yake mjini
Cape Town iliyopewa jina la de Klerk ilisema rais huyo wa zamani alipatwa
maradhi ya kizunguzungu baada ya kurejea nyumbani Jumapili kutoka safari ya
Ulaya, na kuonana na daktari wake Jumatatu.
"Alikuwa na matatizo kama hayo katika
wiki za hivi karibuni na daktari wake alishauri upachikwaji haraka wa
kifaa cha kurekebisha mapigo ya moyo.
"Atapachikiwa kifaa cha kurekebisha
mapigo ya moyo baadaye leo (jana) na atakaa hospitalini hapo usiku mzima,"
taasisi hiyo ilisema katika taarifa yake.
Rais wa Afrika Kusini alitoa taarifa jana
akimtakia kiongozi huyo wa zamani kupona kwa haraka.
"Tunamtakia Rais huyo wa zamani afya
njema katika kipindi hiki kigumu. Wacha tumweke yeye na familia yake katika
mawazo yetu na maombi," alisema Jacob Zuma.
Jumamosi iliyopita taasisi hiyo ilitoa
taarifa kwa niaba ya de Klerk na mkewe, Elita, ikisema waliamua kuahirisha
ziara ya kikazi na mapumziko barani Ulaya sababu Mandela anaumwa sana, na
kwamba walikuwa wakimwombea kiongozi huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi aimarike
afya yake.
Mandela alipelekwa hospitali moja ya
Pretoria Juni 8, mwaka huu kutibiwa kile ambacho serikali ilisema wakati huo
kurejea kwa maambukizi kwenye mapafu.
Tangu hapo, hali yake imeendelea kuwa tete
nchini Afrika Kusini na duniani kote kwa mtu huyo aliyetumikia miaka 27 jela
kabla ya kuja kuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo katika uchaguzi huru mwaka 1994.
De Klerk, waziri wa zamani wa elimu ambaye
alirejesha ubaguzi wa shule, alikuwa muhimu katika kipindi kigumu cha mpito
ambacho kiligeuka na kuwa cha amani licha ya hofu ya kusambaa kwa mapigano ya
kibaguzi.
Mwaka 1990, mwaka mmoja baada ya kuwa Rais
wa Afrika Kusini, akatangaza kukitambua chama cha African National Congress,
kundi lililopigwa marufuku ambalo liliongoza harakati za kupinga ubaguzi wa
rangi, na kuwezesha kuachiwa huru kwa Mandela.
Alitunukiwa Tuzo ya Noble sambamba na
Mandela kwa juhudi zake za kimapinduzi na kwa haraka kuamua mwenyewe
kuachia madaraka.
De Klerk baadaye alishika wadhifa wa
makamu wa rais wakati wa awamu moja ya miaka mitano ya Mandela akiwa rais.
Tangu kustaafu kwake kutoka maisha ya
siasa, amekuwa akisafiri kila kona na kutoa mafundisho.
Taasisi yake inasema malengo yake ni
kusaidia mafukara na watoto wasiojiweza, kushiriki kutatua migogoro na kulinda
kikamilifu katiba ya Afrika Kusini, ambayo inasaidia kulinda haki za binadamu.
0 comments:
Post a Comment